Mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri,“Mfumo huu utasaidia kupunguza muda, kuondoa urasimu uliokuwepo kwa baadhi ya sehemu,” Kitali alisema kwenye mahojiano hayo. “Na sehemu nyingine tulikuwa tunaambiwa kwamba kuna rushwa tumepunguza kwa sababu hukutani moja kwa moja na mwananchi.”Mfumo huo pia humsaidia mteja kujihudumia mwenyewe, hali ambayo haimlazimu tena kwenda ofisi za halmashauri kuomba, au kulipia, tozo, ushuru, leseni, faini au vibali mbalimbali badala yake anaweza kufanya mwenyewe kupitia dirisha la mteja, au Taxpayer Portal.
Hapo awali Kata ya Buzuruga haikuwa na shule ya kata ya sekondari ambapo iliwabidi wanafunzi wa maeneo hayo kutembea umbali mrefu kwenda shule za jirani kama kangae kutafuta elimu, Kupitia fedha za SEQUIP shilingi Milioni 470 ikapatikana shule mpya ya sekondari ya Buzuruga ambapo ilijengwa miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, maabara,jengo la utawala,jengo la TEHAMA na matundu ya vyoo.Haikushia hapo mwaka 2022 kupitia fedha kutoka serikali kuu Shule ya Sekondari Buzuruga ilipata fedha kiasi cha Shilingi Milioni 280 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 14 pamoja na meza na viti 700.
UWEPO WA MIUNDOMBINU BORA YA KUJIFUNZA NA KUJIFUNZIA ILEMELA WANAFUNZI, WAZAZI NA WALIMU WAMSHUKURU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.DKT SAMIA SULUHU HASSAN
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.