Miradi iliyokaguliwa ni ya sekta za afya, elimu na viwanda na biashara lengo ikiwa ni kujiridhisha maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo ili itakapokamilika iweze kuleta tija kwa wananchi wa Ilemela.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na; ujenzi wa paa soko la sabasaba, ukamilishaji wa ujenzi zahanati ya bwiru, ujenzi wa madarasa matatu (03), matundu sita (06) ya vyoo elimu msingi, ujenzi wa madarasa mawili (02) na matundu sita (06) ya vyoo elimu ya awali na ukarabati wa shule ya msingi kitangiri, Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) kituo cha afya kitangiri uendelezaji wa ujenzi wa ofisi ya kata ya kirumba, ujenzi wa chumba kimoja (01) cha darasa shule ya sekondari kabuhoro na ukamilishaji wa Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Msingi Tumaini.
Wataalam hao wakiongozwa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Dkt. Maria Kapinga kwa pamoja waliridhishwa na maendeleo ya miradi kwa kiasi kikubwa na kutoa ushauri kwa mapungufu yaliyojitokeza huku wakihimiza ukamilishaji wa miradi hiyo katika muda uliopangwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.