Tarehe 02/12/2025 kupitia mkutano wa kwanza wa halmashauri, madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025, waliapishwa rasmi zoezi lilioenda sambamba na uchaguzi wa mstahiki meya na naibu meya wa Manispaa ya Ilemela.
Kufuatia uchaguzi huo Mh. Sara Ngw’ahni diwani wa kata ya Buswelu kupitia CCM amechaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela kwa kupata kura 27 kati ya kura zote 27 zilizopigwa huku Mh. Kuluthum Abdallah diwani wa viti maalum kupitia CCM amechaguliwa kuwa Naibu Meya kwa kupata 23 na kumshinda mgombea mwenzake ambae ni Mh. Donald Ndaro diwani wa kata ya Kitangiri kupitia chama cha ACT – WAZALENDO ambae alipata kura 4 kati ya kura 27 zilizopigwa.
Zoezi hili lilisimamiwa na Bi. Anna Mbao katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela ambapo na kuwataka kuhakikisha wanakuwa kiunganishi sahihi kati ya serikali na wananchi kwa kusikiliza changamoto zote za wananchi na kuzipeleka kwa serikali kupitia vikao vya baraza la madiwani ili ziweze kutatulia na hatimae wananchi waweze kupata maendeleo.
Kuapishwa kwa madiwani, pamoja na kumchagua mstahiki meya na naibu meya sambamba na kuunda kamati za kudumu za halmashauri ni hatua ya kuanza kutekeleza majukumu ya baraza katika halmashauri kwenye kuwatumikia wananchi wa Ilemela.
Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ilemela linaundwa na madiwani 27, ambapo madiwani 7 ni wa viti maalum, 19 ni wa kata , pamoja na mbunge wa Jimbo la Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.