Halmashauri ya Manispaa Ilemela ilianzishwa kwa Sheria ya Serikali za Mitaa Na. 8 ya mwaka 1982 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002. Kwa Tangazo la Serikali Na. 256 la tarehe 28/11/2011 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilitangazwa rasmi tangu 01 Oktoba, 2012.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ipo upande wa Kusini mwa Ziwa Victoria. Magharibi imepakana na Ziwa Victoria, Mashariki imepakana na Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Kusini Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Halmashauri hii ipo kati ya Latitudo, 2015’ na 2031’ Kusini mwa mstari wa Ikweta, na ipo kati ya Longitudo 320 45’ na 330 Mashariki. Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ni kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Mwanza. Halmashauri zingine ni pamoja na Halmashauri ya Ukerewe, Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Halmashauri ya Buchosa na Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina ukubwa wa eneo lipatalo kilomita za mraba 1080.55. Kati ya hizo kilomita za mraba 828.45 (76.7%) zimefunikwa na maji na kilomita mraba 252.10 (23.3%) ni nchi kavu. Eneo la Manispaa ya Ilemela ni sawa na asilimia 3.1 ya eneo lote la Mkoa wa Mwanza ambalo ni kilomita za mraba 35,187 ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 20,095 ni nchi kavu na kilomita za mraba 15,092 ni maji ya Ziwa Victoria.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina tarafa 1, kata 19 na mitaa 171. Kwa upande wa majimbo ya uchaguzi, Halmashauri ina jimbo 1 la uchaguzi ambalo Mbunge wake anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula. Aidha, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla ya Waheshimiwa Madiwani 26 ambao miongoni mwao Madiwani wa kuchaguliwa ni 19 na wakuteuliwa ni 7. Wilaya ina jumla ya watumishi wa umma 3,305 wakiwemo wanaume 1,327 na wanawake 1,978
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.