Mhe Amiri Mkalipa, Mkuu wa wilaya ya Ilemela amewataka wataalam wa lishe kuhakikisha wanasimamia vyema masuala ya lishe ili kuweza kuwa na jamii yenye lishe bora.
Ametoa rai hiyo wakati akiongoza kikao cha tathimini ya lishe wilaya siku ya tarehe 22 Januari 2026, kikao kilicholenga kujadili taarifa ya nusu mwaka katika kipindi cha Julai - Desemba 2025/2026
Aidha Mhe Mkalipa, amewataka wataalam wa lishe kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa chakula kinachopikwa ili kuepukana na magonjwa mbalimbali sambamba na kuchukua hatua kwa wale wote ambao watakikuka taratibu.
Nao wajumbe wa kikao hicho katika nyakati tofauti wamepongeza jitihada za kitengo cha lishe katika kutekeleza shughuli za lishe katika kipindi cha Julai - Desemba 2025/2026 huku wakiwataka watendaji wa kata kuwashirikisha madiwani kushiriki katika maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya mtaa (SALIM).
Akiwasilisha taarifa ya hali ya lishe kwa nusu mwaka Bi Pili Kassim ambae ni afisa lishe wa Manispaa ya Ilemela alisema kuwa,kitengo kinaendelea kufanya maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya mtaa katika jamii ili kuzidi kuwaibua watoto wenye changamoto ya utapiamlo na kutoa huduma stahiki ikienda sambamba na kutoa elimu ya kutosha juu ya uandaaji na mpangilio wa chakula unaofaa kwa kutumia vyakula vinavyowazunguka katika maeneo yao wakizingatia makundi sita ya chakula
Kupitia kikao hicho cha tathmini ya lishe wilaya taarifa mbalimbali kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai - Desemba 2025/2026) zilijadiliwa ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe, ukaguzi wa chakula, kupitia na kujadili kadi alama ya lishe, taarifa ya ulaji wa chakula shuleni,maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya mtaa na taarifa ya hali ya lishe,
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.