Kata ya ibungilo ni miongoni mwa kata 19 ambazo zinaunda halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla ya mitaa saba(7) imeanza kufanya kazi wakati wa uchaguzi mwaka 2015.Kata hii imezaliwa toka kata ya Nyamanoro.Kata hii imepakana na kata ya kawekamo kwa upande wa mashariki,Magharibi inapakana na kata ya Nyamanoro na kitangiri,Kaskazini imepakana na kata ya Pasiansi na kusini imepakan na kata ya Nyasaka.Kata ina jumla ya wakazi 24070 na kaya 5917 wanaume wakiwa 11,050 na wanawake 13,020 kwa sensa mwaka 2022
shughuli za kiuchumi katika kata ya Ibungilo ni kilimo,biashara,ajira ikiwemo watu walioajiriwa na serikali na baadhi ya waajiriwa wa mashirika binafsi.
Kata ya Ibungilo ina masoko mawili Nyamanoro na soko la Kiloleli.Wafanya biashara hufanya biashara kutoka kata yetu na kata za Halmashauri ya Ilemela na Nyamagana,Soko la Kiloleli limezidi kuzorota,wafanyabiashara waliopo ni wachache upande wa vibanda vya wafanyabiashara ndogondogo na maduka,maduka mengi yamefungwa Kwa sababu hali ya biashara sio nzuri katika soko hili.
DIWANI : HUSSEIN MAGERA
MTENDAJI WA KATA: BERNADETHA CHARLES
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.