UTANGULIZI
Kata ya Bugogwa ni miongoni mwa Kata kumi na tisa (19) zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoa wa Mwanza. Upande wa Mashariki imepakana na Kata ya Sangabuye, Kusini na Magharibi imepakana na Kata ya Shibula, na upande wa Kaskazini imepakana na Ziwa Victoria.
Kata ya Bugogwa ina jumla ya mitaa kumi na tano (15), kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 kata ina jumla ya kaya elfu saba mia moja na nane (7,108) zenye jumla ya wakazi 38,698, KE 22,666 na ME 16,032
.MUUNDO WA UTAWALA NA UONGOZI:
Kata ya Bugogwa inaye kiongozi ambaye ni Mh. Diwani anayetokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Steven William Mashamba aliyeshinda katika uchaguzi mwaka 2020 na viongozi wa Mitaa. Na Mtendaji wa Kata ni Ndugu Aloyce Mkono
TAASISI ZA UMMA:
Kata ya Bugogwa inazo taasisi kama
Kituo cha Polisi Igombe,
Kituo cha Afya Karume,
Shule ya Sekondari Bugogwa,
Shule ya Sekondari Kisundi,
Shule ya sekondari Igogwe,
Shule ya Msingi Isanzu,
Shule ya Msingi Kilabela,
Shule ya Msingi Kabangaja,
Shule ya Msingi Kisundi,
Shule ya Msingi Igombe,
Shule ya Msingi Bugogwa na
Shule ya Msingi Kayenze ndogo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.