Jumla ya watahiniwa 7912 (Wavulana 3801 na wasichana 4111) waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2025 katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wameanza rasmi mtihani huo utakaofanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 17 Novemba hadi 05 Disemba mwaka 2025.
Kati ya watahiniwa 7912, watahiniwa 7691 ni watahiniwa wa shule (wavulana ni 3695 na wasichana ni 3996)na upande wa watahiniwa binafsi ni 221 (wavulana wakiwa 106 na wasichana ni 115).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Bi. Ummy Wayayu, kwa niaba ya uongozi wa Ilemela anatoa rai kwa wazazi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao ili waweze kufanya mitihani yao kikamilifu na amewaasa watahiniwa wote kuepukana na aina yoyote ya udanganyifu kwani wameandaliwa kikamilifu sambamba na kufuata taratibu, miongozo na sheria zote za mitihani.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla ya vituo 66 vya kufanyia mtihani, kati ya hivyo vituo 55 vikiwa ni vituo vya shule na vituo 11 ni vya watahiniwa binafsi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.