MAJUKUMU YA SEKTA YA KILIMO
Kutoa mafunzo ya kanuni bora za kilimo kwa wakulima ikiwemo upandaji kwa nafasi na kwa wakati, matumizi ya pembejeo, zana na teknolojia za kisasa, teknolojia za umwagiliaji na kilimo hai. Mafunzo haya yanatolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo mihadhara, mijadala, mashamba darasa na mashamba ya mfano.
Kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo ya kilimo kwa kupanga na kugawa matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji kwa eneo.
Kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo, mfano ni wapi pembejeo zinapatikana, hali ya masoko, uwezesho wa kifedha na hata mashirika yanayowasaidia wakulima kupata mahitaji yao mbalimbali
Kuwasaidia wakulima kuanzisha na kutunza vitalu vya mbegu za mboga na matunda kwa ajili ya kukuza mazao ya bustani
Kufanya maonesho mbalimbali kupitia siku za wakulima, na hata ngazi ya wilaya kupitia maonesho ya nanenane.
Kutoa mafunzo ya hifadhi ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika na matumizi ya viuatilifu vya mazao ya kilimo ghalani.
Kuwatembelea wakulima, kuona changamoto wanazokutana nazo na kutoa ushauri wa jinsi ya kutatua changamoto hizo.
Kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wakulima ili kuwahamasisha wenzao kupenda kufanya vizuri zaidi. Hii inaleta ushindani ambao hatimae unasababisha ongezeko la uzalishaji kwa ujumla
Sekta ya Mifugo na Uvuvi ni miongoni mwa sekta muhimu za Halmashauri ya Mji wa Geita. Idara hii inafanya kazi zake kwa kuakisi Dira na dhima ya Halmashauri ya Mji Geita ambayo nia yake kuu ni kuinua maisha ya wananchi kwa kutoa huduma bora na kuinua uchumi wa wananchi katika Mji wa Geita na Taifa kwa ujumla.
Sekta hii imeundwa na sehemu mbili ambazo ni:
i. Sekta ya Mifugo
ii. Sekta ya Uvuvi
Kazi za Sekta ya Mifugo na Uvuvi
Miongoni mwa kazi za Sekta ya Mifugo na Uvuvi ni kama ifuatavyo;
1. Kuhakikisha usalama wa chakula na lishe bora unakuwepo katika ngazi ya kaya,
2. Kuwajengea uwezo wafugaji juu ya ufugaji bora,
3. Kuboresha miundo mbinu ya Mifugo na Samaki kwenye kata husika,
4. Kusimamia kanuni za ufugaji bora ili kuhakikisha kuwa wafugaji wanazalisha kwa tija ukilinganisha na mifugo na maeneo waliyonayo.
5. Ukusanyaji wa mapato yatokanayo Machinjio na Vyanzo vingine vya mapato idara ya Mifugo na Uvuvi.
6. Kuboresha Mifugo,Samaki na mazao yake kwenye maeneo husika,
7. Kutoa elimu ya ugani kwa wafugaji wa Mifugo na samaki,
8. Kuhakikisha usalama wa chakula na lishe bora unakuwepo katika ngazi ya kaya,
9. Kuboresha miundo mbinu ya Mifugo na Uvuvi kwenye Kata husika,
10. Kusimamia sheria na kanuni za Mifugo na Uvuvi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.