Songa na Dokta Samia Suluhu Hassan, sasa ni Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Halmashauri ya Manispaa Ilemela ilianzishwa kwa Sheria ya Serikali za Mitaa Namba. 8 ya mwaka 1982 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kwa Tangazo la Serikali Namba. 256 la tarehe 28/11/2011 na kutangazwa rasmi tarehe 01 Oktoba, 2012 kuwa Halmashauri ya Manispaa Ilemela.Halmashauri ya Manispaa Ilemela ina tarafa 1 na kata 19, mitaa 171 ikiundwa na baraza la madiwani lenye jumla ya madiwani 26, na mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Angeline Mabula wote kutoka CCM.Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ipo upande wa Kusini mwa Ziwa Victoria. Magharibi imepakana na Ziwa Victoria, Mashariki imepakana na Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Kusini Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Halmashauri hii ni kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Mwanza. ukubwa wake, ni kilomita za mraba 1080.55. Asilimia 76.7 za eneo lake zimefunikwa na maji na asiimia 23.3% ni nchi kavu. Eneo la Manispaa ya Ilemela ni sawa na asilimia 3.1 ya eneo lote la Mkoa wa Mwanza.Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imeendelea kupokea fedha kutoka serikali kuu, kwa ajili wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.Katika kipindi cha miaka mitatu cha awamu ya sita kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2024 chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE DKT SAMIA SULUHU HASSAN, Halmashauri imepokea jumla ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 65.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Kiasi cha Shilingi Bilioni 16.67 zimepokelewa katika sekta ya Elimu Sekondari, Bilioni 6.65 katika sekta ya Elimu Awali na msingi, Bilioni 3.2 sekta ya Afya na Bilioni 1.75 ukamilishaji wa jengo la utawala.Bado tunasonga na Mama Samia hapa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, katika kipindi hiki cha miaka mitatu fedha zingine zilizopokelewa ni kiasi cha Shilingi Bilioni 13.79 zimepokelewa kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi wa kimkakati wa stendi ya mabasi ya Nyamhongolo, Bilioni 5.39 kwa utekelezaji wa miradi ya TASAF, Bilioni 3.58 zoezi la upimaji wa ardhi sangabuye.Si hivyo tu kiasi cha Bilioni 1 zimepokelewa ikiwa ni fedha za msaada wa kibajeti na Milioni 227.91 zilipelekwa katika mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuchochea maendeleo ndani ya jimbo la Ilemela.Aidha Bilioni 12.90 ambazo ni fedha za mapato ya ndani zimetekeleza miradi mbalimbali ya Afya, Elimu, uvuvi, upimaji na ulipaji wa fidia za ardhi, maendeleo ya jamii, barabara, masoko na biasharaHII NDIO MIAKA 3 YA SONGA NA SAMIA.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.