Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka watendaji wa wizara ya Afya na wadau wa afya nchini kusimamia utekelezaji wa afua na misingi iliyopangwa kwenye andiko la mradi pandemic fund ikienda sambamba na usimamizi mzuri wa fedha ili kuimarisha uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga ya kiafya ili kufanikisha malengo yaliyopangwa.
Ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Oktoba, 2025 Mkoani Mwanza wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa 'Pandemic Fund' unaolenga kuimarisha uwezo wa kuzuia, kujitayarisha, kugundua na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na dharura nyingine za afya ya jamii nchini ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia aprili 2025 hadi Machi 2028.
Katika kufanikisha hayo Dkt. Biteko amezielekeza sekta zote zinazohusika kusimamia kikamilifu shughuli zake zote ili kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa na haitarajiwi kuwe na mipango mingine huku akiwahakikishia ushirikiano kutoka serikalini ili mradi huu uweze kukamilika na kutoa matokeo chanya.
Nae Dkt Grace Magembe Mganga Mkuu wa Serikali amesema kiasi cha dola 138.7 za kimarekani zimewekezwa katika mradi huu pandemic fund, fedha ambazo zimechangiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mashirika ya kimataifa yakiwemo WHO,UNICEF na FAO, ambazo zitatekelezwa na wizara za afya, mifugo na asasi mbalimbali za afya zikilenga kuimarisha udhibiti katika maeneo yenye muingiliano, kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa maji safi na salama, kuimarisha upatikanaji wa mawasiliano, sambamba na kuimarisha maabara za vipimo.
Mradi huu utashughulikia maeneo matatu ya kipaumbele kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za afya za kimataifa za mwaka 2005. Maeneo hayo ni kuimarisha mifumo katika Kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na dharura za kiafya; kutoa tahadhari za mapema na mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa; mifumo ya maabara kwa sekta za binadamu na wanyama; Kuimarisha rasilimali watu na uwezo wa wafanyakazi katika sekta ya afya na wanyama
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.