Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii inaunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto kupitia mpango kazi wa serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).
Akizungumza katika kikao cha kukumbushana namna ya shughuli za mpango wa MTAKUWWA zinavyofanyika mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii manispaa ya Ilemela ndugu Sitta Singibala amesema
“Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya kutokomeza unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto imejipanga vizuri katika kuhakikisha elimu kubwa ya uelewa inatolewa huku vyombo husika vya kushughulikia matukio hayo vikishirikishwa kwa ukaribu ili kuwezesha mawasiliano ya haraka na kwa wakati katika kuondoa kabisa matukio ya unyanyasaji ndani ya jamii ya Ilemela.ukatili wa kijinsia Ilemela sasa basi”
Nae Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali KIVULINI ndugu Yassin Ally amesema ni muhimu kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao muda mwingi na kuwalea watoto katika mazingira rafiki ya kuwafanya wawe huru kuzungumza pindi wanapokuwa na jambo lolote la kuwatatiza.
“Wazazi wengi hatuna utaratibu mzuri wa kuongea na watoto wetu katika kuhakikisha kwamba mtoto anakuwa huru kuongea chochote.Viongozi wa dini muongoze katika kukemea vitendo hivi kwa jamii.Wapo viongozi wasio waadilifu ambao pia ni wahusika katika matukio ya ukatili.Tusinyamaze.”
Akihitimisha kikao hicho mratibu wa mradi wa MTAKUWWA wa Ilemela Bi.Sarah amesema “Tumejipanga vizuri kwa mipango madhubuti kwa kutumia muongozo wa taifa wa MTAKUWWA wa mwaka 2017/18 – 2021/22.Ni wakati wa kupaza sauti zetu kwa ajili ya kutetea jamii yetu ya Ilemela.”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.