JAMII YAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KATIKA UNYONYESHAJI NA MAKUZI YA MTOTO
"Juhudi za kumfanya mtoto aweze kunyonya na kupata afya bora sio jukumu la mama peke yake, kina baba, jamii na wadau mbalimbali tunapaswa tushirikiane"
Rai hiyo imetolewa na Bi Rose Nyemele muuguzi mkuu wa Manispaa ya Ilemela akimwakilisha mganga mkuu wa Manispaa ya Ilemela katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama yaliyofanyika katika kituo cha Afya Buzuruga leo Tarehe 07.08.2025.
Akizungumza na kina mama waliokuja kupatiwa huduma ya mama na mtoto katika kituo hicho Bi Rose amewashukuru wazazi, walezi, watoa huduma za afya na wadau mbalimbali kwa ushiriki wao uliopelekea maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kuwa yenye mafanikio.
Bi. Pilli Khasim, Afisa lishe wa manispaa ya Ilemela akisoma taarifa ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama amesema kuwa lilikuwa ni kutoa elimu ya unyonyeshaji kwa watu 13,724 ambapo tangu kuanza kwa maadhimisho haya tarehe 01.08.2025 na hadi kufikia kilele leo tarehe 07.08.2025 amesema kuwa watu 13,961 sawa na 102% wamefikiwa, kati yao wakina mama ni 13,961 na wakina baba ni 65 tu
Akizungumza kwa niaba ya wazazi Ndg. Faraji Issa mkazi wa mtaa wa Ilalila amewashukuru wataalam kwa kutoa elimu ya unyonyeshaji maziwa ya mama na pia amewahimiza kina baba wenzake kuwa mstari wa mbele kuwasaidia kina mama katika malezi ya watoto pamoja na kuhudhuria mafunzo na huduma mbali mbali za kiafya zinazotolewa kwa watoto.
Maadhimisho haya ya wiki ya unyonyesha wa maziwa ya mama ni ya 33 tangu kuanzishwa kwake na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Thamini unyonyeshaji, weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.