Hayo yamebainishwa siku ya tarehe 19 Agosti 2025 na Ndg Leonard Robert ambae ni mratibu wa TASAF manispaa ya Ilemela ambapo amefafanunua zaidi kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitano,( 2020 - 2025 ) Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilipokea jumla ya Tsh. 6,898,449,620.00 (Shilingi Bilioni 6.89) ambapo kaya 4,652 zimenufaika na mpango huu ikiwa ni wastani wa kaya zote toka kuanza kwa zoezi hili.
Nae Bw. Fidelis Kirayo mwezeshaji wa mtaa wa Kaguhwa kata ya Nyamhongolo amewasihi wanufaika wa mpango huu kuwa mabalozi wazuri na kuweza kuendelea kushirikiana katika vikundi vyao walivyojiunga ili kuweza kupata mikopo ya halmashauri na kujikwamua kutoka katika umaskini.
“Tuendelee kuwa mabalozi kwa kuwaeleza wananchi juu ya mipango mbalimbali ya serikali kuhusiana na kuondoa umaskini na tuendelee kupambana tusaidie na wengine kuonyesha kwamba tulitumia mbinu hii kujikwamua kiuchumi” alisema Bw. Kirayo Mwezeshaji TASAF
Naye Bi Tereza Pius kwa niaba ya wanufaika ameishukuru serikali kwa mpango wa TASAF kwa kuweza kumsaidia kujikwamua kimaisha kwani ameweza kutoka kuishi kwenye nyumba ya nyasi mpaka kupata nyumba ya bati na kuendesha familia yake kiujumla.
“Nilikuwa naishi kwenye nyumba ya nyasi na nilikuwa navujiwa kila mara ila TASAF imenisaidia sana nikanunua bati nikaezeka nyumba yangu kutoka kwenye fedha za TASAF na sasa hivi naishi kwenye nyumba ya bati sipati shida tena ya kuvujiwa,”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.