Jumla ya maafisa waandikishaji 60 wa mfuko wa bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) iliyoboreshwa wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo mpya wa malipo kwa njia ya kielektroniki (kwa kutumia namba ya kumbukumbu) yaani ‘control number’
Wakiwa katika mafunzo hayo wametakiwa kufanya kazi ya uandikishaji kwa umakini, uadilifu wa hali ya juu. Kauli iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Ndugu John Wanga alipokuwa akifungua mafunzo hayo.
“Niwatake mkafanye kazi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu kwani sitarajii kusikia afisa mwandikishaji anachukua fedha na kuziweka mfukoni,”Alisisitiza.
Aliongeza kusema kuwa, lengo la mpango huu ni kuwafanya wananchi wanapata huduma bora wakati wote iwapo ana pesa au hana pesa, hivyo nizidi kuwasisitiza kuwa hata nyie ni vyema mkajiunga na bima hii kwani ni nzuri.
Pamoja na hayo aliwataka maafisa wasimamizi ambao ni maafisa maendeleo ya jamii kuhakikisha wanaelimisha jamii ili iweze kuona na kutambua umuhimu wa bima hii na ili wananchi waweze kupata huduma hii kwa urahisi.
Mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboreshwa (CHF) katika manispaa ya Ilemela unatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa malipo wa kielektroniki ambapo mwanachama atapatiwa namba ya kumbukumbu (control number) kwa ajili ya kufanya malipo.
Lengo la mfumo huu mpya ni kupunguza na kuondoa kabisa upotevu wa fedha uliokuwa ukitokea katika mfumo wa malipo ya zamani, Alisema mratibu wa bima ya afya iliyoboreshwa Ndugu Leonard
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.