Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mapema leo wamepatiwa elimu kuhusiana na namna ya kukabiliana na majanga ya moto katika taasisi n ahata katika nyumba zao.
Akitoa elimu hiyo Mkuu wa Zimamoto na uokoaji wa Wilaya ya Ilemela, Inspekta Deus Rutta aliwaonyesha kwa vitendo namna ya kuvitumia vifaa vya kuzimia moto vilivyopo na huku akisisitiza kuwa hutakiwi kukimbia moto unapotokea bali kuzingatia mafunzo waliyopatiwa.
Alifafanua aina za moto zilizopo na kuwa zipo katika madaraja tofauti, na kuwa sio kila kizimio cha moto kitazima aina yoyote ya moto.Aidha alisisitiza kuwa moto unapotokea kuhakikisha kuwa umeme umezimwa mara pindi moto unapotokea na sio kutumia maji kuzima moto huo hali ya kuwa umeme bado unawaka.
Halikadhalika alielezea namna ya kuzima moto unaotokana na gesi huku akisisitiza kuwaelimisha wasichana wa kazi wanaoachwa majumbani kuhusiana na matumizi mazuri ya gesi ili kuweza kuepukana na majanga ya moto ambayo kwa sasa yamekithiri.
“Takriban asilimia 80 ya majanga yanayotokea kwa sasa ni yanayotokana na gesi hivyo ni vizuri kwenda kuwaelimisha na wasichana wa kazi mnaowaacha majumbani juu ya elimu hii ya namna ya kukabiliana na moto na kuhakikisha matumizi mazuri ya vifaa vya moto ikiwemo ges”, Amesema
Pamoja na hayo amewataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanapojenga nyumba za kuishi ni vizuri kukawepo mlango wa dharura wa kutokea pindi janga la moto linapotokea ili kuepusha madhara yatokanayo na moto ikiwa ni pamoja na kifo.
Mmoja wa watumishi alimshukuru Inspekta Rutta kwa elimu hiyo yenye manufaa kwa taasisi na hata majumbani huku akiwaomba kuendelea kutoa elimu hii katika taasisi mbalimbali hususan katika shule zilizopo wilayani na kwingine.
Akihitimisha mafunzo hayoambapo watumishi walipata fursa ya kufanya majaribio, pia amewataka kueneza elimu hii ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto, na kusema kuwa kitengo chao cha zimamoto na uokoaji hutoa elimu hii bure popote pale wanapoitwa na huku akitoa namba ya kupiga iwapo moto umetokea kuwa ni 114
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.