Zikiwa zimesalia siku 31 kufikia uchaguzi mkuu 2025 wa Rais, wabunge na madiwani Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza imeendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika octoba 29 mwaka huu.
Kupitia tamasha la Visit Ilemela ambalo limefanyika tarehe 28 Septemba 2025, katika mwalo wa Igombe kata ya Bugogwa wananchi mbalimbali hususan wavuvi wa mwalo huo wamefikiwa na elimu ya umuhimu wa kushiriki uchaguzi mkuu ambapo kwa upande wao wananchi waliojitokeza kupata elimu hiyo wameipongeza INEC -Ilemela kwa kuwapatie elimu hiyo.
Miongoni mwa elimu waliyopewa wananchi hao wakiwemo wavuvi ni uwezekano wa kupiga kura ya rais hata kama wapo nje ya kituo walichojiandikishia kupiga kura na wananchi 20 wameweza kubadilisha kituo cha kupigia kura
Akizungumza wakati wa utoaji elimu hiyo katika kata ya Bugogwa jimboni humo, Afisa uchaguzi wa Manispaa ya Ilemela, Shilinde Malyagili amesema tume huru ya uchaguzi imetoa ruhusa ya wananchi kupiga kura ya Rais katika vituo tofauti na walivyojiandikishia.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.