Lishe bora maana yake ni kula chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kusaidia mwili kukua vyema, kuwa na afya na uwezo na kuupa mwili nguvu ya kupambana na magonjwa, kuharakisha ukuaji wa mtoto na mwili kuwa na kinga.
Kwa kutambua umuhimu wa lishe bora kwa mama na mtoto leo tarehe 12/09/2025 watoa huduma ya kliniki na kinga (CTC) na huduma ya mama mtoto (RCH) wa manispaa ya Ilemela wamepatiwa mafunzo ya lishe bora kwa mama na mtoto.
“Lengo kuu la mafunzo haya ni kuhakikisha huduma za kilishe zinafanya vizuri na tunategemea baada ya mafunzo haya huduma za kilishe zitaimarika katika vituo vyetu vya kutolea huduma,” Amesema Pili Kassim Afisa lishe wa Manispaa ya Ilemela.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo Bi. Damarice Dawson muuguzi msaidizi kutoka kituo cha Afya Buzuruga amewashukuru wawezeshaji kwa mafunzo waliyopata kwani yamewaongezea ufahamu kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo lishe bora kwa mama na mtoto.
"Tumejifunza kwa vitendo namna ya kuwatambua watoto wenye udumavu wa kawaida na uliopitiliza kwa kutumia njia ya kuwapima watoto uzito ,urefu au mzingo wa mkono, tutahakikisha elimu hii tunaitumia kuboresha afya za watoto",amesema Bi Damarice
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.