Katika kuhakikisha wananchi wanashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 katika hali ya amani na utulivu msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ilemela, Ndg Herbert Bilia ameendelea kukutana na makundi mbalimbali yaliyopo ndani ya wilaya ya Ilemela ikiwa ni muendelezo wa kutoa hamasa ya uelewa juu ya uchaguzi na mambo ya muhimu ya kuzingatia kuelekea uchaguzi mkuu.
Akifungua semina ya elimu ya mpiga kura kwa viongozi wa maafisa usafirishaji pamoja na wavuvi siku ya Alhamisi ya tarehe 11 Septemba 2025, Ndg. Bilia,amelitaka kundi hilo kuungana kama taifa moja kulinda amani ya nchi ikiwa ni pamoja na kushiriki kampeni zinazoendelea kwa lengo la kusikiliza sera za wagombea ili kuweza kuchagua viongozi bora.
"Tumewaita hapa ili tuungane kama taifa moja kushiriki kampeni zinazoendelea kwa kusikiliza sera za wagombea lakini kuwaasa tusitumike katika vihatarishi vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu kwani yapo maisha baada ya uchaguzi",amesema Ndg Bilia
Kwa upande wake Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ndg. Shilinde Malyagili, amesema vijana wengi wamejiajiri katika sekta isiyo rasmi ambayo inachangia asilimia 50 ya pato la taifa hivyo wanatakiwa kutambua umuhimu wa kuchagua viongozi bora watakao waletea maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Nao washiriki wa semina hiyo wamesema kuwa elimu waliyoipata imewajengea uelewa mkubwa wa kutambua umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Tarehe 29, ockoba 2025
Wajibu wetu kama viongozi wa makundi haya ni kutunza amani na kupitia vikao vyetu kuwahimiza wanachama wetu kuhudhuria kampeni mbalimbali zinazoendelea ili kuweza kuchagua viongozi sahihi wanaoweza kutuletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kujitokeza kupiga kura ifikapo tarehe 29 oktoba 2025, sisi maafisa usafirishaji na makundi mengine tusitumike vibaya kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani", amesema Abdulrashid Sudi, katibu wa bodaboda kata ya shibula
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.