Takribani watoto 66396 wamefikiwa na watoa huduma za afya katika kampeni ya kitaifa ya mwezi wa afya na lishe ya mtoto ikiwa ni sawa na asilimia 100.2 ya lengo lililokuwa limewekwa la kufikia watoto 66,381.
Kupitia kampeni hiyo, kitengo cha lishe chini ya Idara ya Afya Ilemela kilikadiria kuwafikia watoto 66381 kati yao, 9,022 wa miezi 6 hadi 11 na watoto 57,359 ni wa miezi 12 hadi 59.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukagua maendeleo ya ugawaji wa matone hayo afisa lishe wa manispaa ya Ilemela Bi Pili Kasimu amesema kuwa hadi kufikia tarehe 28 Juni 2024, watoto 9034 wa miezi 6 hadi 11 na watoto 57,362 wa miezi 12 hadi 59 sawa na jumla ya watoto 66,396 ikiwa ni asilimia mia moja ya lengo lililokuwa limekusudiwa walikuwa wamepatiwa matone ya vitamin A
Aidha Bi Pili amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwapeleka watoto katika vituo vya kutolea huduma hata baada ya kampeni hiyo kwa kuwa huduma hiyo itakuwa ikiendelea kutolewa vituoni kama kawaida sanjari na kuendelea kuwatoa hofu wazazi na walezi juu ya usalama wa huduma hiyo
Bi Esha Mahizo Mtoa huduma wa zahanati za Nyerere iliyopo kata ya Buswelu na Bi Enisa Mbilinyi kutoka zahanati ya kata ya Kahama wametoa pongezi kwa viongozi wa Serikali za mitaa yao kwa kuhamasisha wananchi kujitokeza na kushiriki zoezi hilo kwa wingi wakaongeza kusema kuwa utekelezaji wa ugawaji wa matone ya vitamin 'A' katika maeneo yao
Kwa upande wake mzazi wa mtoto Grecious Nyagabona Bi Justina Michael mbali na kuwasisitiza wazazi wenzake kuwaleta watoto vituoni kupata matone ya vitamin 'A' ameiomba serikali kuendelea na kampeni mbalimbali za namna hiyo kwani zinasaidia kutoa msisitizo kwa wazazi na walezi kuwaleta watoto vituoni kupata na huduma nyingine za kiafya
Kampeni ya kitaifa ya mwezi wa afya na lishe chini ya kauli mbiu “Matone ya Vitamin A ni Bora kwa Ukuaji Watoto wetu”, imedumu kwa mwezi mmoja ambapo watoto wote waliofika katika vituo vya kutolea huduma wamefikiwa na wengine kufuatwa katika maeneo yao kwa kufanya outreach (Huduma za mkoba) na maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe ya Mtaa (SALIM).
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.