Ikiwa ni siku ya pili tokea muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2024 kuanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe CPA Amos Makalla amefika katika shule za msingi na sekondari ndani ya Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kujionea maendeleo ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza, darasa la kwanza na awali sambamba na kukagua miundombinu ya shule mpya.
Mhe Makalla ametumia ziara hiyo kuongea na wanafunzi wa shule za sekondari na msingi ndani ya Manispaa ya Ilemela na kuwataka kuzingatia masomo kwani kilichowapeleka shuleni hapo ni kusoma na kupata maarifa. Sambamba na hilo amewahimiza kupendana na kushirikiana katika kila jambo.
“Mzingatie sana kitu elimu, ndio kitu ambacho mzazi wako amekuleta hapa usome upate maarifa”Amesema CPA Makalla
Aidha Mhe Makalla ametoa rai kwa wazazi kuhakikisha wanafunzi waliopangiwa kuanza kidato cha kwanza wanaripoti shule na kuwapeleka wanafunzi wa awali na darasa la kwanza kwa ajili ya kuwaandikisha na kusisitiza kuwa kwa sasa hakuna kisingizio cha kukosa ada kwani rais wa jamhuri wa muungano wa tanzania ameweka unafuu kwa kufuta ad azote kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita.
“Hakuna kisingizio cha mwanafunzi kukosa ada, kwani ada kalipa Mhe Samia Suluhu Hassan”, Amesema CPA Makalla
Zaujath Najim, ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule mpya ya Sekondari Kisenga, yeye kwa niaba ya wanafunzi wenzake amefurahishwa kuchaguliwa kujiunga katika shule hiyo na akatumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwani wamekuta miundombinu mizuri ikiwa na meza na viti hivyo hakuna mwanafunzi anaekaa chini, alisema.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.