Katibu Mkuu Kiongozi OR-TAMISEMI, Ndugu Joseph Nyamhanga amemuagiza Mkurugenzi wa Ilemela kuanza ujenzi wa Hospitaali ya Wilaya kwa haraka.
Ametoa malekezo hayo alipokuwa katika ziara ya kikazi ambapo ailfika kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani hapa ikiwa ni mara ya kwanza toka alipoteuliwa kushika nafasi hiyo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiwa eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi a Hospitali hiyo lililopo kata ya Bugogwa Mtaa wa Isanzu, Katibu Mkuu alitoa maelekezo hayo kuwa ujenzi unatakiwa kuanza haraka ili kuweza kumaliza kwa wakati uliokusudiwa kwani muda wa ujenzi ni miezi sita.
Katika ziara hiyo alikutana pia na timu ya menejimenti na kutoa maelekezo mbalimbali huku akisisitiza suala la ukusanyaji mapato kwa kutumia mashine za kielektroniki ili kudhibiti upotevu wa mapato.
Pamoja na hayo amempongeza Mkurugenzi John Wanga na timu ya menejimenti kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ambayo aliitembelea.
Katibu Mkuu OR-TAMISEMI amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Manispaa ya Ilemela ikiwemo eneo la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,kituo cha afya Karume,ujenzi wa shule ya sekondari Kayenze.Miradi mingine aliyokagua ni pamoja na mradi wa barabara za kiseke-sabasaba-Buswelu pamoja na ujenzi wa madarasa 3 na matundu 10 ya vyoo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.