KAMATI YA UKIMWI ILEMELA YATEMBELEA VIKUNDI VYA WAVIU Katika kuhakikisha dhamira na jitihada zinazochukuliwa na Manispaa ya Ilemela za kupambana na kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi na madhara yake kwa Jamii zinazaa matunda, Kamati ya kudhibiti UKIMWI imefanya ziara kwa vikundi vya WAVIU kwa ajili ya kuhakiki namna ya vikundi hivyo vinavyotumia ruzuku wanayopewa na Manispaa kwa uanzishwaji wa miradi mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi na kuacha utegemezi sambamba na kujua changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa Ilemela Mheshimiwa Shaban Maganga amevitaka vikundi hivyo kuwa na matumizi sahihi ya ruzuku wanayopewa kwa kutekeleza miradi waliyoikusudia awali na kuacha kubadilisha miradi hiyo kiholela pasi na kushirikisha Manispaa sanjari na kuagiza wataalamu wa Halmashauri kufanya uhakiki wa kutosha na kutoa elimu kwa vikundi kabla ya kuwapatia fedha hizo … Ni muhimu sasa wataalamu muwe mnatoa Elimu na kufanya uhakiki kwa Vikundi kabla ya kuwapatia fedha zenu kwa maana ya mapato yanayotokana na kulipa kwenu kodi niwaombe mtumie vizuri fedha hizi…’ Aidha Mheshimiwa Maganga amewahakikishia WAVIU hao kuwa Manispaa yake itaendelea kuunga mkono shughuli zinazofanywa na Vikundi vyao na kuwataka kuacha kujiona wanyonge kwa kutojishughulisha na Kazi yeyote halali ya kujiingizia kipato Wawakilishi wa vikundi hivyo wameishukuru Kamati hiyo na Manispaa ya Ilemela kiujumla kwa uamuzi wake wa kuvitembelea Vikundi hivyo na kuahidi kuongeza jitihada katika kuongeza jitihada katika kufanya kazi na kujikwamua kiuchumi ili kuacha utegemezi huku wakiomba kutatuliwa kwa haraka kwa changamoto zinazowakabili ikiwemo kukutanishwa na wadau wa kudhibiti ujasiriamali sambamba na wadau wa kudhibiti ubora wa bidhaa jambo ambalo Mheshimiwa Maganga aliwahakikishia litafanyika na kutoa maelekezo kwa wataalamu juu ya utekelezaji wake Ziara hiyo ilifanyika tarehe 14/02/2017 na kutembelea vikundi vya WAVIU vya Neema Yatosha cha Kawekamo-Nyasaka, Wanguna cha Nyamanoro-Mkudi, Lwidima cha Kirumba na Umoja wa Matumaini cha Ibungilo-Mchongomani.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.