ZAIDI YA WATOTO 92,409 WANUFAIKA NA DAWA ZA KINGA YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO
Zaidi ya watoto 92,409 wanaoishi wilaya ya Ilemela wamenufaika na zoezi la umezeshwaji wa dawa za kukinga na kutibu ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo ikiwa ni mkakati wa Serikali katika kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Hayo yamesemwa na Bi Gisela Orasa mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD) kutoka wilaya ya Ilemela wakati wa uzinduzi wa kampeni ya umezeshaji wa dawa za kukinga na kutibu ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo kwa wanafunzi wa shule za umma na binafsi na kata zote Kumi na Tisa zilizopo Ilemela zoezi lililofanyika katika shule ya msingi Isenga Kata ya Pasiansi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
“ Lengo kuu ni kutoa chanjo ya kuzuia magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo kwa watoto walio chini ya miaka mine mpaka kumi na nne na tunategemea kuwafikia watoto zaidi ya Elfu Tisini na Mbili Mia Nne na Tisa”, Alisema.
Aidha ameongeza kuwa zoezi hilo kwa Manispaa ya Ilemela limetekelezwa kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Idara ya Elimu na ni zoezi shirikishi likihusisha si watoto wa mashuleni tu hata waliopo manyumbani wenye umri huo wa miaka minne mpaka kumi na nne
Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya msingi Isenga Pasiansi akiwemo Emmanuel Majala na Salma Moshi wa darasa la saba shuleni hapo mbali na kushiriki katika kumeza dawa hizo wameishukuru Serikali kwa kuanzisha mpango huo wenye lengo la kupambana na magonjwa yaliyosahaulika ingawa yamekuwa na madhara makubwa kwao kunakosababisha vifo kwa watoto wengi na kukatisha ndoto zao huku wakitaka kuongezwa kwa muda wa utoaji wa umezeshwaji wa dawa hizo ili kuwafikia watoto enzao waliowengi mitaani
Nae mratibu wa zoezi hilo kutoka Idara ya Elimu Mwalimu Witness Mugyabuso amesema kuwa zoezi la umezeshaji wa dawa za kichocho na minyoo ya tumbo kwa shule za msingi za umma na binafsi ndani ya wilaya yake limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia Themanini pamoja na baadhi ya changamoto zilizojitokeza ikiwemo ushirikiano mdogo kutoka kwa wazazi kwa kutowapa chakula watoto ili waweze kumeza dawa na kusababisha mzio (aleji) kwa wanafunzi waliopata dawa bila kula akiwemo mmoja kutoka shule ya msingi Pasiansi na kukimbizwa haraka zahanati ya Pasiansi kwa matibabu zaidi.
Zoezi hilo lilizinduliwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa John Mongella ambapo lilizinduliwa katika shule ya msingi Isenga iliyopo katika manispaa ya Ilemela
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.