Kiasi cha shilingi milioni sitini na laki tatu na elfu tisini na sita kutoka katika fedha za mfuko wa jimbo zimetumika kwaajili ya kuchochea shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya jimbo la Ilemela .
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza walimu wa shule za sekondari kwa kupata matokeo mazuri kitaaluma Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa jimbo lake limepokea kiasi hicho cha fedha kwaajili ya shughuli za kimaendeleo ambapo shilingi milioni 30 ilitumika kwaajili ya kununua gari aina ya Mitsubish Delicia yenye usajili namba SM 14564 itakayotumika kwaajili ya kusafirishia wataalam wanaofanya kazi katika maeneo yasiyofikika kiurahisi au shughuli za misiba inapojitokeza katika jamii huku kiasi cha shilingi milioni 27 ikitumika kwaajili ya ununuzi wa samani za ofisi kwa walimu wa shule 27 za Sekondari za Serikali, milioni 4.5 ikitumika kwaajili ya ununuzi wa seti tatu za kompyuta kwa shule 3 za Sekondari zilizofanya vizuri ikiwemo Bwiru wavulana, Kilimani na Nyasaka, milioni 9 ikitumika kutengeneza madawati 120 ambayo yatagawanywa kwa shule 4 za msingi zenye uhaba mkubwa na milioni 13 na elfu 50 zikitumika kwaajili ya ununuzi wa mifuko 580 ya saruji itakayozalisha tofali 23,200 ambayo yatagawanywa kwa ajili ya kujenga maboma ya ofisi za mitaa17
‘.. Lengo langu ni kuleta motisha ya ushindani kielimu, tutagawa japo kwa uwakilishi kidogo tulichopata mbele ya wenye duka kwa maana ya wenye Ilani ya uchaguzi chama cha mapinduzi ili wajue katika kata zao tumefanya nini ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula amemshukuru Rais Mhe Samia Suluhu Hasan kwa fedha za maendeleo alizozitoa katika jimbo lake ambapo ndani ya mwaka mmoja zaidi ya bilioni 30 zimekwisha tolewa huku akiwataka wananchi wa jimbo hilo kumpongeza na kumuombea kiongozi huyo ambae pia ni mlezi wa wilaya ya Ilemela
Kwa upande wake mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga mbali na kumpongeza mbunge huyo ameahidi kuisimamia manispaa hiyo kupitia baraza lake la madiwani katika kuhakikisha fedha zinazoletwa na Serikali zinatumika kama zilivyokusudiwa ili miradi iweze kukamilika kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati sahihi
Nae kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo Ndugu Sitta Singibala amemshukuru mbunge huyo pamoja na kuahidi ushirikiano katika kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya manispaa hiyo itakayosaidia kupunguza changamoto mbalimbali kwa wananchi
Wasinyo Werema ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Bwiru wavulana kwa sasa ambae amemshukuru mbunge wa jimbo la Ilemela pamoja na kumpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya katika kusukuma gurudumu la maendeleo huku akitaja baadhi ya manufaa aliyoyapata akiwa mkuu wa shule mbili kwa nyakati tofauti kutoka kwa mbunge huyo ikiwemo taulo za kike alizozitoa shule ya sekondari Sangabuye yeye akiwa mwalimu mkuu na futari kwa wanafunzi wa shule ya Bwiru yeye pia akiwa mwalimu mkuu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.