Wananchi wa Manispaa ya wametakiwa kujitokeza kwenye mikutano ya kliniki za ardhi katika kata zao kw aajili ya kusikilizwa na kutatuliwa kero, migogoro na changamoto za ardhi walizonazo
Hayo yamesemwa na kamishna wa ardhi msaidizi mkoa wa Mwanza Bi Happiness Mtutwa wakati wa muendelezo wa kliniki ya ardhi katika viwanja vya shule ya sekondari Lumala kata ya Ilemela inayofanywa na idara ya ardhi manispaa ya Ilemela kwa ajili ya utatuzi wa changamoto mbalimbali za ardhi ambapo amewasisitiza wananchi kutumia fursa ya uwepo wa kliniki na kujitokeza kuwasilisha changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi
‘.. Nitoe wito na rai kwa wananchi wanaposikia matangazo ya uwepo wa kliniki hizi kujitokeza kuwasilisha kero zao, Sisi kama mkoa tunatamani kero na changamoto zote za ardhi za mkoa wa Mwanza ziweze kuisha,’ Alisema
Aidha Kamishna msaidizi Bi Mtutwa ameipongeza manispaa ya Ilemela na uongozi wake kwa kuweka utaratibu wa kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwani mkoa huo una halmashauri nyingi lakini ni Ilemela pekee inayofanya vizuri katika mkoa huo kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuzifikia kata zote na kwamba ofisi ya ardhi mkoa wa Mwanza itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha malalamiko yote ya wananchi yanafanyiwa kazi na kutatuliwa
Kwa upande wake mkuu wa idara ya ardhi manispaa ya Ilemela Bi Grace Masawe amesema kuwa idara yake imeweka mpango wa kuzifikia kata zote za manispaa hiyo kwa kila siku ya ijumaa ya wiki ili kusikiliza kero, changamoto, malalamiko, ushauri, elimu ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi, kutoa elimu ya kodi za ardhi na masuala yote yanayohusu ardhi ikiwemo matumizi ya ardhi, upimaji, ujenzi ili kuwaondolea wananchi usumbufu na gharama za kuwafuata wataalam katika ofisi zao
Charles Steven ambae ni mkazi wa mtaa wa Lumala kata ya Ilemela ambae kero yake kero yake ya umikilishwaji imeweza kutatuliwa pamoja na kushukuru kwa ushauri aliopewa na wataalam amewahimiza wananchi wenzake kutopuuza matangazo yanapotolewa ya uwepo wa wataalam katika maeneo yao katika kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.