WILAYA YA ILEMELA YAKABIDHIWA MRADI WA MAJI WA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 80
Wilaya ya Ilemela imekabidhiwa mradi wa maji wenye thamani ya Tsh Milioni 80 kutoka katika kampuni ya bia ya Serengeti.
Mradi huu wa maji safi utahudumia takriban wananchi 7560 wa Mtaa wa Kaghua katika kata ya Nyamhongolo na unao uwezo wa kuzalisha maji lita 4000 kwa saa.
Akizindua mradi huo Mhe Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dr.Angeline Mabula ameushukuru uongozi wa kampuni ya bia Serengeti na kusema kuwa amefarijika kuona kuwa ipo mstari wa mbele katika kusaidia maeneo yanayoigusa jamii yetu moja kwa moja.
“Ni dhahiri kuwa chanzo cha maji kilichopo hakikuweza kutoshelea mahitaji ya eneoo letu na hivyo basi kuona umuhimu wa kuchimba kisima ili kuweza kutosheleza mahitaji ya maji ya wakazi wa hapa”, Alisema
Aidha ametoa wito kwa uongozi na wananchi wa eneo hilo kuhakikisha kuwa mradi huu unalindwa ili kuufaya kuwa endelevu kwa ustawi wa jamii husika.
Nae Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo ndugu John Wanyancha, alisema kuwa mradi huo ujulikanao kama maji ni uhai hautasaidia tu kuboresha afya za wakazi wa eneo hilo , bali utaongeza uzalishaji mali kwa kuwa wasichana na akina mama hawatatembea tena umbali mreu kutafuta maji na kuongeza kuwa utawapa wasichana muda zaidi wa kuhudhuria shule.
Akiushukuru Uongozi wa kampuni ya bia Serengeti Mtendaji wa kata ya Nyamhongolo kwa niaba ya wananchi, aliahidi kuwa watautunza mradi huo na kuulinda kwa kushirikiana na kamati ya maji iliyoundwa ili kuhakikisha mradi huo unabaki katika ubora wake
Mradi huu wa maji umejengwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa kushirikiana na shirika la AMREF ikiwa ni jitihada za Mhe mbunge wa jimbo la Ilemela katika kutatua changamoto za wananchi wake.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.