• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

WATUMISHI ILEMELA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

Posted on: September 16th, 2022

Watumishi wa makao makuu ya halmashauri ya manispaa ya Ilemela wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata maadili ya utumishi wa  umma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa divisheni ya utawala na rasilimali watu manispaa ya Ilemela Bi.Leokadia Humera wakati wa kikao kazi na watumishi Manispaa ya Ilemela ambacho kilikuwa na lengo la kuwakumbusha watumishi juu ya haki na wajibu wao katika utumishi wa umma sambamba na kusikiliza na kupokea kero zao kwa lengo la kuboresha utendaji kazi utakaoleta matokeo chanya.

Akiwasilisha mada kuhusu wajibu na haki ya mtumishi wa umma Bi. Humera amezitaja haki mbalimbali za mtumishi wa umma ikiwemo likizo ya mwaka kwa kila mtumishi,haki ya kustaafu na mafao stahiki, sambamba na haki ya kupata matibabu kwa mujibu wa kanuni na sheria za kazi kwa watumishi wa umma.

‘.. Ni muhimu watumishi wote wa umma kufahamu haki na wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwani wataweza kuepuka mambo yasiyofaa  na kutenda yale yanayotakiwa  kwa mlengo wa kutoa huduma bora kwa wananchi tunaowahudumia ..’

Aidha amefafanua kwa undani kanuni na sheria za kazi zinazomtaka mtumishi kutimiza wajibu wake kama kuwahi kazini, kuwepo kazini muda wote wa kazi na kuepuka utoro na kubainisha makosa mepesi na mazito na adhabu zake.


“Ni wajibu wa watumishi wote wa umma kufanya kazi kwa ushirikiano,upendo na kuepuka makundi yasiyofaa kwa lengo la kutoa huduma kwa wateja wetu na sisi wenyewe kuweza kuwajibika ipasavyo katika nafasi zetu kwa amani. “ amesema Bi. Humera.


Akihitimisha kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Joseph Apolinary amesema ni wajibu wa kila mtumishi kutambua nafasi yake katika utendaji na kuahidi kuendelea kutoa nafasi ya vikao kama hivyo kwa watumishi wote wa Halmashauri kwa maslahi mapana ya ustawi wa manispaa ya Ilemela pamoja na kuahidi kufanyia kazi ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na watumishi hao katika kikao kazi hicho.

Mayala Nyanda ni mmoja wa watumishi waliohudhuria kikao hicho yeye anashukuru kwa utaratibu huu wa watumishi kupewa elimu juu ya wajibu na haki zao kwani utasaidia watumishi kutobweteka na kufanya kazi za viwango vinavyokubalika kila siku.

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • WALENGWA TASAF WAASWA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA VIKUNDI

    April 28, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.