Watumishi wa Manispaa ya Ilemela wameshauriwa kujipenda kwa kuhakikisha wanapima Afya zao mara kwa mara.
Hayo yamesemwa na Afisa lishe wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Bi.Pili Khasim wakati wa zoezi la kawaida la tathimini ya hali ya lishe kwa watumishi wa Manispaa hiyo linalofanyika kila baada ya miezi mitatu katika ukumbi wa Manispaa kwa kutoa vipimo mbalimbali vya kiafya.
" Kazi zetu ni kuwahudumia wananchi ni muhimu tuwe vizuri kiafya kuweza kuwahudumia kwa ufanisi."
Bi.Pili ameongeza kuwa idara ya Afya kupitia kitengo cha lishe kimeweka utaratibu wa kuwasogezea huduma za upimaji watumishi wa Manispaa kwa vipimo mbalimbali kama presha, HIV ,sukari, urefu na uzito sambamba na ushauri wa kitaalamu wa bure wa masuala ya afya ikiwemo ushauri wa magonjwa yasiyoambukiza kutokana na watumishi wengi kubanwa na majukumu ya kiofisi.
Seif Sufian ni dereva wa Manispaa ya Ilemela yeye ameshukuru kitengo cha lishe na uongozi wa Manispaa kwa kuona umuhimu wa watumishi kupima afya zao.
" Kufahamu afya zetu ni vizuri kwani inatupa uelekeo wa namna ya kuendelea kuishi,kama ni mgonjwa uendelee kujifuatilia na kama ni mzima uzidi kujilinda." Amesema Seif
Huduma hizo zinaendelea kutolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ndani ya Manispaa ya Ilemela, wananchi wote mnasisitizwa kufika kupata huduma za kitaalamu kulingana na mahitaji yenu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.