Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Mhe AmirI Mkalipa amesisitiza juu ya kufanyika kwa vikao vya wazazi mashuleni kwa ajili ya kuwahamasisha na kuwahimiza wazazi kuhakikisha wanachangia chakula ili watoto wao waweze kupata chakula.
Ametoa rai hiyo wakati akiongoza kikao cha tathmini ya lishe wilaya siku ya alhamisi 13 Novemba 2025, kikao kilichofanyika kwa ajili ya kujadili taarifa ya Julai - Septemba 2025/26

Aidha Mhe Mkalipa amewataka watendaji wa kata kuhakikisha maafisa ugani kilimo katika kila kata wanasimamia mashamba na bustani katika shule ambazo zina maeneo kwa ajili ya kilimo, ili kuwezesha upatikanaji wa chakula mashuleni.
Wakijadili taarifa ya ukaguzi wa chakula, wajumbe walishauri kuendelea kutolewa elimu kwa wananchi namna bora ya kuepukana na magonjwa ya mlipuko, ambapo mkaguzi chakula ndugu Francis Dougan amesema kuwa kati ya mafanikio waliyoyapata ni pamoja na kuzifikia shule 38 na wauza vyakula 268 ambapo waliwapatia elimu ya usalama wa chakula.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha Julai - Septemba 2025/26, Bi Pili Kassim ambae ni afisa lishe wa manispaa ya Ilemela, alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 30 zilitumika kutekeleza shughuli za lishe ambapo jumla ya shughuli 12 zimetekelezwa ikiwemo mafunzo kazini kwa watoa huduma 28, maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji pamoja na shughuli zingine
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.