• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

WATOTO WAMETAKIWA KUTOA TAARIFA ZA UNYANYASAJI WANAOFANYIWA

Posted on: June 16th, 2025

Ikiwa ni siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka siku ya tarehe 16 mwezi juni, watoto wa wilaya ya Ilemela wameungana na mataifa mengine barani Afrika kuadhimisha siku ikiwa ni kumbukizi ya maandamano ya watoto wa soweto, Afrika Kusini mwaka 1976 ambapo walipinga suala la ubaguzi wakipambania haki zao za msingi.

 

Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuongeza uelewa kuhusu hali ya watoto wa afrika na kuhimiza utekelezaji wa haki zao kama ilivyoainishwa katika ibara ya 2 hadi ya 22 ya mkataba wa Afrika wa haki na ustawi wa mtoto.

 

Chini ya Kauli mbiu ya mwaka huu  2025 inayosema “Haki za Mtoto; Tulipotoka, Tulipo na Tuendako”, inawataka wazazi, walezi, serikali na wadau wengine mbalimbali kutathmini mafanikio yaliyopatikana na changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa haki za mtoto,kwa  kuzingatia wajibu wao katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na maendeleo ya Mtoto.

 

Akimwakilisha aliyekuwa mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe Hassan Masala, Bi Anna Mbao Afisa Tawala wa wilaya ya Ilemela amewapongeza watoto hao kwa kuadhimisha siku yao hii muhimu na kusisitiza kuwa jukumu la ulinzi wa mtoto linaanza na mtoto mwenyewe hivyo kuwataka wasisite kuzipigania haki zao kwa kutoa taarifa kwa wakati pale haki zao zinapokiukwa na kuhakikisha wanajilinda na kutambua misingi wanayotakiwa kuishi.

 

"Serikali inatambua umuhimu wa watoto ndio maana imeweka miongozo na sheria  mbalimbali ,kwa ajili ya kuwalinda na kuwatetea watoto ili tuweze kupata watoto wenye akili wanaojitambua watakayoyaishi wanayoelekezwa ili tutengeneze taifa bora la baadae, hivyo mkaishi elimu mliyopatiwa", amesisitiza Bi Anna

 

Nae mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela Bi Ummy Wayayu amewaasa na kuwataka watoto kuwa  walinzi wa kwanza wa unyanyasaji wanaofanyiwa kabla ya watu wengine kuwa walinzi kwao kwa sababu wao ndio waathirika wa kwanza wa unyanyasaji

 

Kupitia Risala ya watoto iliyosomwa na mtoto Aziza Malilo kwa niaba ya watoto wenzake wameiomba serikali kuendelea kupambana na kuongeza nguvu zaidi katika kutekeleza haki za watoto, kupatiwa elimu pasipo kubaguliwa sambamba na kuendelea kuwekeza katika watoto

 

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika wilaya ya Ilemela kwa mwaka 2025 yalipambwa na matukio mbalimbali kama vile bunge la watoto ambapo walipata fursa ya kuzielezea changamoto zao, sambamba na kwaya, maonyesho , na shairi.

 

 

 

Announcements

  • TANGAZO LA KAZI NAFASI YA UDEREVA DARAJA LA II June 04, 2025
  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • ILEMELA YAPONGEZWA KUPATA HATI SAFI, WITO WATOLEWA KUTOZALISHA HOJA MPYA ZA UKAGUZI

    June 17, 2025
  • WATOTO WAMETAKIWA KUTOA TAARIFA ZA UNYANYASAJI WANAOFANYIWA

    June 16, 2025
  • MHE MASALA ASISITIZA HAMASA YA LISHE SHULENI

    June 04, 2025
  • "TUUFANYE USAFI KUWA NI TABIA YA KUDUMUA": ANNA MBAO

    May 31, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.