Watendaji wa kata za manispaa ya Ilemela wametakiwa kutoa kipaumbele katika suala la lishe kwa kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa wazazi/walezi kuchangia lishe mashuleni kupitia mikutano ya hadhara,vikao vya wazazi mashuleni n.k
Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Mhe Hassan Masala akiongozaa kikao cha tathmini ya lishe wilaya siku ya tarehe 10 machi 2025.
“Tunapotoa chakula kwa watoto wetu, tunawajengea mazingira mazuri ya kuzingatia masomo yao, mtoto anapopata lishe na ubongo wake unaimarika” alisema Mhe Masala.
Sambamba na maelekezo hayo, amewaelekeza wafanyabiashara kuweka utaratibu wa kutembelea masoko pamoja na kutoa elimuu kwa wafanyabiashara ili waweze kurudi katika maeneo waliyotengewa na sio kufanyia biashara barabarani.
Aidha Mhe Masala amekipongeza kitengo cha lishe manispaa ya Ilemela kwa jitihada ambazo wamekuwa wakiendelea nazo za kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa lishe ambapo imepelekea Ilemela kuongoza kimkoa katika agenda ya lishe.
Nae afisa lishe wa manispaa ya Ilemela, amewasihi watendaji wa kata kuhakikisha pembe inapulizwa katika mitaa yao ili jamii iweze kujitokeza wakati wa maadhimisho ya zoezi la siku ya afya na lishe ya mtaa (SALIM) huku akitaka wanaume kuhimizwa kushiriki zoezi hilo kwani litawawezesha kupata uelewa wa lishe hasa kwa Watoto wao.
Kikao hicho cha tathmini ya lishe wilaya kilienda sambamba na zoezi la upimaji wa afya kwa wajumbe wa kikao hicho zoezi lililoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela , Mhe Hassan Masala.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.