Watendaji wa kata na Mitaa wa Manispaa ya Ilemela wametakiwa kuwa chachu katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya serikali
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary wakati wa kikao kazi na watendaji hao kilicholenga kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024
"Niwatake mkawe mstari wa mbele katika kusimamia suala zima la ukusanyaji wa mapato ya serikali ili tuweze kufikia malengo yaliyowekwa pamoja na kutekeleza shughuli mbalimbali za Serikali, amesisitiza Eng.Modest
Aidha amewataka watendaji hao kusimamia vyanzo mbalimbali vya mapato kwa uaminifu ili kuzitendea haki nafasi walizoaminiwa nazo kwa kushirikiana na wenyeviti wao wa mitaa.
Pamoja na hayo Mkurugenzi amewataka watendaji hao kusimamia vyema fedha za miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao kwa kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ikiwa inaakisi thamani ya fedha.
Nae Mweka Hazina wa Manispaa amewahimiza suala zima la ushirikiano katika suala zima la ukusanyaji mapato ili kuweza kufikia malengo na kuwahimiza kuwa wakaitishe vikao katika kata zao kwa ajili ya kutoa elimu ya ukusanyaji mapato.
Aloyce Mkono ambae ni mtendaji wa Kata ya Bugogwa kwa niaba ya watendaji wenzake pamoja na kushukuru kwa kikao kazi hicho aliomba na watendaji kukumbukwa katika ziara mbalimbali za mafunzo ili nao waweze kuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali hususan namna watendaji wenzao wanashiriki katika ukusanyaji mapato.
Akihitimisha kikao hicho Mkurugenzi amewasisitiza watendaji kuwasikiliza wananchi na kutoa huduma bora.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.