Watendaji wa kata na mitaa wa Manispa ya Ilemela wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika maeneo yao kwa kuhakikisha jamii zinatambua na kuchukua tahadhari zote muhimu juu ya namna ya kujihadhari na ugonnjwa wa kipindupindu sambamba na kufahamu sheria zinazoweza kuchukuliwa kwa mwananchi atakayepinga jitihada za serikali katika kupambana na kipindupindu.
Akizungumza wakati wa kikao cha dharura kwa ajili ya kuwakumbusha watendaji hao juu ya kuhamasisha jamii kutokujisahau kwa kuweka mazingira safi na kufuata sheria zilizopo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwl.Marco Busungu amewataka watendaji hao kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha kuwa kila nyumba ina choo bora na kinatumiwa ipasavyo.
Mwl.Busungu amewataka wote wanaochuruzisha maji machafu nyakati za mvua kuacha mara moja na minada isiyo rasmi kufungwa na kusisitiza uwepo wa maji safi ya kunawa maeneo yote ya biashara na makazi na kusisitiza faini zitatozwa kwa wote watakaokwenda kinyume na taratibu na sheria zilizopo.
“Tunahitaji kushikamana kwa janga hili tulilonalo,kila mmoja awajibike kwenye eneo lake kuhakikisha wananchi wanaelewa nini cha kufanya pamoja na sheria zilizopo.Suala hili lisimamiwe kwa umuhimu mkubwa hatupo tayari kuona wananchi wanapotea kwa uzembe wa mtu.” Mwl.Busungu
Nae Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr.Charles Marwa amesema ugonjwa wa kipindupindu unaepukika kwa kuimarisha usafi kwani chanzo chake kikubwa ni ulaji wa kinyesi.
“Tuache uzembe,tuwe wasafi ,tutumie vyoo bora kwa usahihi.”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.