Manispaa ya Ilemela kupitia divisheni ya viwanda, biashara na uwekezaji inaendelea kuwajengea uwezo wataalam wake wa ndani katika kuufahamu na kuleta uelewa wa pamoja juu ya mfumo wa kidijitali wa kuomba leseni za biashara kupitia mtandao (TAUSI).
Kwa kuzingatia nafasi na ukaribu wa watendaji wote wa kata na mitaa walionao kwa wananchi ambao ndio wafanyabiashara wenyewe leo tarehe 25 Julai,2023 Maafisa biashara wa Manispaa wametoa mafunzo kwa watendaji hao kuhusu matumizi bora ya mfumo wa TAUSI .
Wafanyabiashara wote wanapaswa kutumia mfumo huo wa kidijitali katika kufanya maombi ya leseni. Amesema Hashim Kimwaga ambae ni afisa biashara huku akizitaja baadhi ya faida ya mfumo wa TAUSI, kuwa ni pamoja na kuokoa muda wa mfanyabiashara kwani kwa sasa mfanyabiashara anaomba leseni popote pale alipo, inaondoa mianya ya rushwa kwani mfanyabiashara anaomba leseni mtandaoni.
Tangu mwezi Aprili 2023 Manispaa ya Ilemela ilipoanza kutumia mfumo huo wa TAUSI hadi sasa jumla ya leseni 2399 zimetolewa sawa na makusanyo ya shilingi millioni 279.87
Mecktrida Lyimo ni mtendaji wa kata ya Nyamhongolo mmoja wa watendaji waliopata mafunzo leo yeye anatoa shukrani kwa uongozi wa Manispaa kwa kutoa mafunzo hayo kwani wananchi wamekuwa wakifika ofisi za kata na mitaa kupata huduma mbalimbali na kuuliza maswali ya uelewa wa mambo kama hayo.
" Sasa nauelewa mfumo vizuri hivyo hata mwananchi akitaka msaada au uelewa zaidi naweza kumsaidia.Nashukuru kwa uwezeshwaji huu naomba tuendelee kupatiwa uelewa wa pamoja wa masuala mbalimbali ili mambo mengine yaishie ofisi za kata na mitaa kama haina ulazima wa kufika makao makuu ya ofisi za Manispaa."
Ili kujiunga na kufanya maombi hayo ya leseni pamoja na kulipia kwa urahisi tembelea tovuti ya www.tausi.tamisemi.go.tz na ufuate maelekezo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.