"WATENDAJI MTOE ELIMU KWENYE MAENEO YENU." MKURUGENZI UMMY
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bi.Ummy Mohamed Wayayu alipokuwa akizungumza na watendaji wa kata na mitaa yote ya Manispaa hiyo kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kiutendaji.
Amewataka watendaji hao kuwajibika ipasavyo kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato, wananchi wafahamu umuhimu wa wao kuchangia tozo za Halmashauri na elimu ya kujiadhari na magonjwa ya milipuko hasa yale yanayosababishwa na uchafu.
"Tuwaelimishe watu wetu ili tujitengenezee mazingira rahisi katika utendaji kazi wetu,masuala ya tozo za vibali vya ujenzi,leseni za biashara ni muhimu wafahamu kwani makusanyo hayo ndo hutumika katika maboresho ya huduma mbalimbali za kijamii."
Afisa utumishi mkuu wa divisheni ya utumishi ya Manispaa hiyo Egidy amewataka watendaji hao kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake.
Nae Mchumi wa Manispaa hiyo ndugu Albert Bilia amewapongeza na kuwashukuru watendaji kwa ushirikiano mzuri wanaoutoa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya kata zao huku akikiri kuwa ameuona mchango wao mkubwa katika jitihada za kuleta maendeleo ndani ya Manispaa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.