Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kanda ya ziwa, wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa idara ya afya, watendaji wa kata na mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia mfumo wa manunuzi wa kielekroniki, National e-Procurement System of Tanzania (NeST).
Mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 29.05.2025 yakilenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika matumizi sahihi ya mfumo huo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa manunuzi mwandamizi kanda ya ziwa, Ndg. Evaristo Mtilega, ameelezea umuhimu wa matumizi ya mfumo huo ikiwa ni pamoja na uwazi, usiri, thamani ya fedha, uadilifu, ushindindani na uwajibikaji.
Naye Afisa manunuzi msaidizi kanda ya ziwa, Ndg. Jabir Bane amesisitiza wataalam kufuata mtiririko sahihi wa manunuzi ya umma ili kuzuia ubadhilifu pamoja na kubana matumumizi ya fedha za serikali.
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo, mtendaji wa kata ya Sangabuye, Ndg. Egno Mayaka amewashukuru wakufunzi kwa mafunzo mazuri na kuahidi kuyafanyia kazi yote waliyoelekezwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.