Wataalam mbalimbali kutoka idara za afyana elimu wametakiwa kutumia mfumo mpya katika vituo vya kutolea huduma na kuachana na ule wa zamani kwa maana ya njia ya cheki ili kuweza kuendana na teknolojia pia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Rai hii ilitolewa na mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Bi. Ummy Wayayu siku ya tarehe 25.07.2025 wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam hao katika mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa katika vituo vya kutolea huduma (FFARS), yakilenga kutoa uelewa mpana, maarifa na stadi za kuwezesha utendaji wa moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma kama vile shule, zahanati, vituo vya afya na hospitali
“Mfumo huu umekuja kuleta mapinduzi katika mambo ya uhasibu na ukusanyaji wa taarifa hivyo nendeni mkautumie kikamilifu ili kuepukana na changamoto za upotevu wa kumbukumbu za taarifa inayotokana na mifumo ya kizamani ama utengenezwaji wa taarifa za kughushi”. Alisisitiza Bi. Ummy.
Akizungumza wakati akiendesha mafunzo hayo Ndg. Abraham Bisera, muwakilishi kutoka idara ya afya amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia washiriki upata stadi za utunzaji vitabu muhimu vya uhasibu na utunzaji wa kumbukumbu za miamala ya kifedha pamoja na utayarishaji wa taarifa za fedha kwa vipindi mbalimbali.
Naye Ndg. Nkuba Iseni Charles, mtendaji wa kata ya ilemela kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo amemshukuru mkurugenzi na uongozi wa halmashauri kwa kuratibu mafunzo hayo kwani mfumo wa ffars unakwenda kuwarahisia kutekeleza majukumu yao pamoja na kuongezeka kwa ufanisi wa shughuli za kiuhasibu katika maeneo yao ya kazi.
Mfumo jumuishi wa uhasibu na utoaji wa taarifa katika vituo vya kutolea huduma (FFARS) umetayarishwa ili kukidhi mahitaji ya stadi sahihi (zilizoboreshwa) za udhibiti wa fedha katika ngazi ya kituo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.