Mariam Msengi Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela amewataka washiriki wa UMITASHUMTA 2024 kuhakikisha wanakuwa na nidhamu, utiifu na juhudi katika kipindi chote wanachokuwa kambini
Ameyasema hayo tarehe 19 Mei 2024 alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilemela katika ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2024.
"Muwatii wakufunzi na walimu wenu ili mwisho wa siku muweze kufikia ngazi ya mkoa kisha Taifa", alisema Bi Mariam.
Kizito Bahati ni afisa michezo na meneja wa timu Ilemela alisema kuwa lengo ni kuwa wachezaji watakaounda timu ya mkoa ya Mwanza watoke Ilemela.
Aliongezea kwa kusema kuwa takriban wanafunzi 400 wenye umri chini ya miaka 14 wanashiriki mashindano hayo kutoka kanda nne za Bugogwa, Kirumba, Pasiansi na Buswelu.
Isack Malekana ni mshiriki kutoka kanda ya Kirumba anasema amefurahi kushiriki michezo kwani Michezo ni afya, furaha na ajira.
Kauli mbiu:"Miaka 60 ya UMITASHUMTA tunajivunia mafanikio katika sekta ya Elimu, michezo na sanaa, Hima Mtanzania shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024"
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.