Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Said Mtanda amewahimiza wananchi wa Ilemela na mkoa wa Mwanza kwa ujumla kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura zoezi litakaloanza tarehe 11-20 oktoba 2024 ili kuwawezesha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 Novemba 2024.
Aidha ametumia fursa hiyo kutoa elimu juu ya tofauti ya kadi ya mpiga kura na uandikishaji wa daftari la mpiga kura kuwa kadi ya mpiga kura itatumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuwa kadi hiyo haitatumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Sambamba na suala la uchaguzi Mhe Mtanda amewasihi wananchi wa Ilemela kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika sherehe za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2024 zitakazofanyika mkoani Mwanza siku ya Jumatatu ya tarehe 14 Oktoba 2024.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.