"Kwa kipekee niendelee kuwapongeza wananchi kwa kuendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali juu ya haya ambayo tumeletewa katika maeneo yetu, serikali ya Tanzania , inaendelea kuonyesha mapenzi makubwa wananchi kwa kuwafikishia wananchi huduma mbalimbali katika maeneo yao"
Ni kauli ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ndg. Ismail Ali Ussi alipokuwa akiongea na wananchi wa kata ya Nyakato waliofika katika zahanati ya Nyakato siku ya tarehe 26 Agosti 2025,kushuhudia Mwenge wa Uhuru ikizindua wodi ya mama na mtoto.
Aidha Ndg. Ussi amefafanua kuwa mradi huu wa wodi ya mama na mtoto ni miongoni mwa miradi ambayo imenufaika kutokana na fedha za mapato ya ndani za manispaa ya Ilemela na haya yakiwa ni maelekezo ya serikali ya kutenga asilimia 60 ya makusanyo yanatokana na ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
"Jambo kubwa ambalo la kufurahisha ni kwamba wananchi mmeridhia kuyapokea maendeleo haya, wananchi mngekuwa hamjaridhia wodi hii isingekuwepo hivyo ni wajibu wenu wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano madaktari kwani wana kazi ngumu katika taifa hili"alisema Ndugu Ussi
Akisoma taarifa ya mradi huu , mganga mkuu mfawidhi wa zahanati ya Nyakato Daktari Fredrick Mtiba amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa wodi hii kunaenda kupunguza vifo vya mama na mtoto sambamba na kupunguza msongamano katika Kituo cha Afya cha jirani cha Buzuruga ambapo idadi ya wanaojifungua ni wastani wa akina mama 600 hadi 700 kwa mwezi.
Hadi kukamilika kwa ujenzi wa wodi hii shilingi Milioni 227.92 zimetumika kati ya fedha hizo shilingi milioni 24.92 ni nguvu za wananchi zilizotumika kuanzia hatua za maandalizi ya awali na ujenzi wa msingi
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.