Wito umetolewa kwa wananchi wote kutembelea banda la manispaa ya Ilemela katika viwanja vya Nyamhongolo ambapo maonesho ya nanenane 2025 yanaendelea kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali, lakini pia kujipatia bidhaa zilizohifadhiwa katika njia salama zaidi.
Wito huo umetolewa na Mhe Amir Mkalipa, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela alipotembelea maonesho hayo na hususan banda la Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea
"Tumeona kuna uwekezaji mkubwa umefanyika katika kilimo , kuchakata bidhaa za kilimo, kwenye ufugaji na bidhaa za ufugaji hivyo kila mmoja aje kujifunza kilimo bora cha kisasa ufugaji bora wa kisasa lakini namna bora ya kupata bidhaa ambazo zinawekwa katika mfumo wa kiafya zaidi", amesema Mhe Mkalipa
Amewataka pia wananchi kuja kujifunza namna bora ya kufuga kwa vizimba, kuchakata kuanika dagaa namna ya kuhifadhi samaki na dagaa ili zikae muda mrefu,
Aidha Mhe Mkalipa alipotembelea wakulima wa mboga mboga na mazao ya kilimo amewakumbusha pia kulima miche ya viungo ama spices kwa ajili ya afya lakini pia kibiashara
“Uanikaji wa dagaa katika vichanja unasaidia dagaa wasiwe na michanja pia wanakuwa katika hali ya usafi” ni kauli ya Pendo Edward Fikiri mfanya biashara wa dagaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela akitoa hamasa na elimu hiyo katika maonyesho ya Nane 2025
Revocatus ambae ni mtaalam wa kufuga samaki kwa njia ya vizimba ndani ya manispaa ya Ilemela akielezea faida na umuhimu wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba amesema kuwa licha ya kuwa ufugaji kwa njia hii unatoa ajira kwa vijana lakini pia ufugaji rahisi na unaweza kufanyika mahali popote.
Chini ya kauli mbiu isemayo "Chagua viongozi bora kwa maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi 2025 , maonesho ya nanenane kanda ya ziwa magharibi inayohusisha halmashauri za Mkoa wa Mwanza na Geita yanafanyika katika viwanja vya Nyamhongolo ndani ya wilaya ya Ilemela kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.