Wananchi wa Ilemela wameaswa kutumia vyandarua vyenye viatilifu na kuboresha usafi wa mazingira ili kuepuka mazalia ya mbu wanaoleta ugonjwa wa Malaria.
Akizungumza na wananchi wa Ilemela wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria duniani yaliyofanyika kiwilaya kituo cha Afya Karume Mratibu wa Malaria Manispaa ya Ilemela Evaristus Mganga amewaasa wanaIlemela kutumia vyandarua vyenye dawa kila wanapolala ili kujikinga na ugonjwa huo.
,, Wananchi tuachane na imani potofu za kusema vyandarua vyenye dawa ni sumu,vyandarua hivi ni salama kwa matumizi ya binadamu kuzuia ugonjwa wa Malaria na si kwa kufugia mifugo kama baadhi yenu mnavyofanya’’
Aidha ndugu Mganga amesema manispaa ya Ilemela inaendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria kwa njia mbalimbali na kubainisha kuwa jumla ya vyandarua 54020 vyenye viatilifu tayari vimegawiwa kwa wanafunzi 54020 wa shule za msingi ndani ya manispaa sawa na asilimia 100 ya malengo waliojiwekea kwa mwezi Machi ,2022.
Mganga ameongeza kuwa zoezi la utoaji elimu kwa jamii juu ya usafi wa mazingira,kufanya unyunyuziaji wa mazalia ya mbu ili kuua viluwiluwi wanaoeneza Malaria sambamba na ugawaji wa dawa kinga kwa wanawake wajawazito kuzuia maambukizi ya Malaria vinaendelea.
Monika Kashinji ni mkazi wa Igombe anatoa shukrani kwa serikali kuendelea kuwakumbuka wananchi wasio na uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Malaria na magonjwa mengine .
‘’ Kwa kweli mi nashukuru sana na ninafurahi kuona serikali inatambua umuhimu wa kutoa elimu kwa sisi wananchi tusioelewa kuhusu mambo mbalimbali ya afya,elimu iendelee zaidi kwani hata mimi niliwahi kutumia chandarua chang kufugia kuku’’ amesema Monika.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.