WANANCHI WA MANISPAA YA ILEMELA WATAKIWA KUGHARAMIA ZOEZI LA URASIMISHAJI MAKAZI Wananchi wa Manispaa ya Ilemela wametakiwa kugharamia zoezi la urasimishaji wa makazi yao ili kusaidia upangaji wa mji sambamba na kuepuka ujenzi holela usiofuata sheria na taratibu za matumizi ya ardhi Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango Miji wa Manispaa Ilemela Ndugu Kennedy Chigulu alipokuwa Mtaa wa Ibanda kata ya Kirumba baada ya Kamati ya Mipango Miji ya Manispaa hiyo kufanya Ziara yake ya kawaida ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Manispaa hiyo Akizungumza katika ziara hiyo Bwana Chigulu amesema kuwa kwa kawaida Serikali haigharamii zoezi la urasimishaji isipokuwa wananchi wenyewe ndiyo wanagharamia hivyo kazi ya Serikali ni kusimamia zoezi hilo na kuhakikisha taratibu zote za kitaalamu zinafuatwa na kuzingatiwa Hayo yamekuja kufuatia mgogoro wa mipaka uliojitokeza baina ya kata mbili za Kirumba na Kitangiri wakati wa zoezi la urasimishaji linaloendelea katika eneo hilo la Ibanda ambapo amewatahadharisha kuwa suala la kimipangomiji halina mipaka ya kiutawala kwani mchoro unapotoka huwa hauoneshi mipaka ya kiutawala hivyo kwa viongozi na wananchi wanapaswa kuelewa hivyo huku akitaka kukutanishwa kwa pande hizo kutoa elimu ya upimaji shirikishi Kufuatia mgogoro huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Diwani wa Kata Kirumba Mheshimiwa Alex Ngusa amewataka wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha maeneo yote stahiki yanapimwa na kurasimishwa sambamba na kuchangia huku akitanabaisha kuwa Kamati yake haitavumilia mtu yeyote mwenye lengo la kukwamisha zoezi hilo na kuwataka viongozi kukaa na wananchi wao kufanikisha zoezi hilo ‘… Wenyeviti wa Mitaa na Kamati zenu fanyeni vikao na wananchi wa muhakikishe wanachangia zoezi la upimaji na urasimishaji wa makazi yao, Hii ni kwa faida yetu na Sisi hatutamvumilia mtu yeyote atakaekwamisha zoezi hili… Aidha Kamati imewataka Viongozi na wataalam wa Manispaa kuwachukulia hatua wananchi wote wanaofanya shughuli za uharibifu wa mazingira na kuhamasisha upandaji miti ili kutunza mazingira yao kwa faida ya vizazi vijavyo na vya sasa Wajumbe wa kamati hii pamoja watalaam wa Manispaa ya Ilemela walitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo ya mradi wa maji Igombe, ukaguzi wa mazingira kiwanda cha nguo Mwatex, ujenzi wa barabara ya mawe Kawekamo, ujenzi wa daraja Cassanova, na mabadiliko ya matumizi ya ardhi Nyamanoro
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.