Wananchi wa mkoa wa Mwanza wametakiwa kushiriki zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki chaguzi zote za serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Octoba 2024 sambamba na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2025.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda wakati wa hafla ya kilele cha maonesho ya kilimo nane nane katika viwanja vya Nyamhongolo vilivyopo Manispaa ya Ilemela.
" Ni haki na wajibu wa kila mtanzania alie na vigezo vya kupiga kura kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi tunaowataka." Amesema Mhe. Mtanda
Aidha ameongeza kuwa ni lazima viwanja vya Nyamhongolo kufanyiwa maboresho,kuwa na miundo mbinu ya kudumu ili kuleta hamasa zaidi kwa washiriki na kuboresha ulinzi na usalama wa mali za washiriki.
Kabla ya hafla hiyo Mhe.Mtanda alipata fursa ya kutembelea baadhi ya mabanda kujionea bidhaa na vipando vya mazao mbalimbali.
"Banda la Manispaa ya Ilemela limekuwa la tofauti limetufundisha kilimo cha mijini,kilimo kinachotumia nafasi ndogo na kuleta tija kubwa."
Mhe.Mtanda amemkabidhi kikombe cha ushindi wa nafasi ya pili Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bi. Ummy Wayayu kwa Manispaa yake katika kundi la taasisi za serikali za mitaa.
Akihitimisha hafla za maonesho hayo Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhe.Renatus Mulunga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Maonesho ya kanda ya ziwa magharibi yamejumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita huku yakipambwa na kauli mbiu isemayo chagua viongozi bora wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo,uvuvi na ufugaji.
|
|
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.