Wananchi wanaoishi eneo la kando kando ya barabara ya kutoka mjimwema isamilo kuelekea big bites kilimahewa wametakiwa kuilinda, kuitunza pamoja na kuhakikisha wanawachukulia hatua waharibifu watakaojitokeza.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mipango miji na mazingira katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela Mhe Alex Ngusa wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara hiyo na ile ya kutoka Bwiru wavulana sekondari kuelekea Bwiru ziwani ambapo amewapongeza wananchi kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea wilayani humo.
Huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu na kuwachukulia hatua wananchi wenye nia ovu ya kuhujumu kwa kuiba alama za barabarani zilizopo na kuiharibu kwa kuwaripoti katika ngazi za uongozi na madereva wanaotumia njia hiyo kutii na kuheshimu alama ziliwekwa
‘.. Kikubwa tuwaombe wananchi wahakikishe wanaitunza barabara na kuwachukulia hatua waharibifu na wezi wa alama za barabarani ..’ Alisema
Nae mjumbe wa kamati hiyo, Mhe Japhes Rwehumbiza, akatumia ziara hiyo kumtaka mkurugenzi kuwakumbusha wananchi wanaotumia masoko yaliyopo ndani ya wilaya hiyo kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona kwa kuhakikisha wana nawa mikono mara kwa mara, wanavaa barakoa kila wanapoingia sokoni na kupunguza msongamano ili kudhiti maambukizi zaidi ya ugonjwa huo huku mjumbe mwengine ambae pia ni diwani wa kata ya Pasiansi Mhe Rosemary Mayunga akimshukuru mkurugenzi wa manispaa kwa kukubali kutoa milioni moja na laki tano kama ishara ya kuunga mkono jitihada za wananchi katika kuifungua barabara ya kuelekea Bwiru ziwani.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Ndugu Shukran Kyando mbali na kushukuru kwa pongezi zilizotolewa katika ofisi yake, ameahidi kuwa kupitia mamlaka ya barabara za nchi kavu TIRA atazifuatilia gari zinazofanya shughuli za usafirishaji katika barabara ya Isamilo mji mwema ili ziweze kufika mpaka mwisho wa barabara na kuleta tija kwa wananchi sanjari na kuwapongeza wananchi wa Bwiru kwa kuwa wazalendo katika gharama za ufunguzi wa barabara hiyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.