Walimu wa shule za msingi na sekondari wametakiwa kuwasimamia wanafunzi kimaadili na kuwafundisha kwa ufasaha ili kuongeza ufaulu wao katika masomo
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa elimu kutoka Ofisi ya RaisTAMISEMI Mwalimu Dkt Emmanuel S. Shindika wakati wa kikao kazi na walimu wa shule za sekondari na msingi za Serikali na binafsi zinazopatikana ndani ya halmashauri ya manispaa ya Ilemela ambapo amewataka walimu kuhakikisha wanafunzi wanajengewa uwezo wa kusoma kwa ufasaha, kuandika, kusikiliza na kusoma
“Twendeni tukafundishe Ilemela ikae sawa, Wanafunzi wetu wawe wajuzi na uwezo katika nyanja zote” Amesema
Aidha Mwalimu Dkt Shindika akawataka walimu wa wilaya hiyo kuwa na vyanzo vingine vya mapato ili kujiepusha na mikopo umiza inayochangia kuvuruga taaluma kwani badala ya walimu kufundisha wanaanza kuvurugwa na madeni
Kwa upande wake afisa Elimu wa mkoa wa Mwanza Mwalimu Martin Nkwabi amemhakikishia mkurugenzi huyo wa elimu juu ya kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa pamoja na kuboresha taaluma katika shule za sekondari na msingi za mkoa huo
Sitta Singibala akimwakilisha kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela mbali na kuwapongeza walimu wa manispaa hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kufundisha wanafunzi na kuinua taaluma akawataka wataalam wote wanaohusika na utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na mkurugenzi wa elimu kutimiza wajibu wao
Nae Mwalimu Rose Peter kutoka shule ya msingi Kahama ameshukuru kwa kikao hicho cha kujengeana uwezo na kwamba kitawasaidia katika kukumbushana wajibu wao hivyo kuinua taaluma katika manispaa ya Ilemela
Mkurugenzi wa elimu TAMISEMI yupo mkoani Mwanza Kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuboresha sekta ya elimu nchini
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.