Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John.P.Wanga kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe.Dkt.Angeline Mabula wamewapongeza walimu wa Manispaa ya Ilemela wa shule za Sekondari na Msingi kwa ufaulu mzuri katika mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne kwa mwaka 2018.
Sherehe hizo za kuwapongeza ziliambatana na bonanza la michezo pamoja na utoaji wa zawadi na vyeti kwa shule ambazo zilifanya vizuri katika mitihani ya mwaka 2018.
Kwa upande wa shule za Msingi zilizofanya vizuri kwa serikali ni Bwiru,Gedeli na Kitangiri C na kwa shule za binafsi ni Nyamuge, Lowjoma na Ilemela.
Kwa upande wa shule za Sekondari upande wa serikali ni shule za Bwiru Boys,Mwinuko na Nyamanoro na kwa shule binafsi ni Morning Star, Loreto na Marist Boys.
Washindi wa kwanza walipatiwa fedha taslimu Tsh.100,000 jiko la gesi na sukari Kilo 25 ambapo washindi wa pili na watatu walipata jiko la gesi na mfuko wa sukari wa kilo 25 kwa shule zote za Msingi na Sekondari.
Aidha Mhe.Mbunge wa Ilemela pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela wameanzisha mchakato wa upimaji viwanja 1600 katika eneo la Kabusungu kwa ajili ya kuwapatia walimu makazi bora kwa gharama nafuu ya Tsh. 1,500,00 kwa kila kiwanja kikiwa sambasamba na hati na kibali cha ujenzi.
Mwaka 2018, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela iliongoza kimkoa kwa kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya darasa la saba na kidato cha nne ambapo kitaifa matokeo ya darasa lasaba ilishika nafasi ya sita ikitokea nafasi ya 20 na kwa upande wa elimu sekondari ilishika nafasi ya 17 kitaifa ikitokea nafasi ya 19.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.