Afisa ufuatiliaji mradi wa kupunguza kaya maskini Tanzania (TASAF) Wilaya ya Ilemela Alex Kabona amewaasa walengwa wote kuwa na mpangilio mzuri wa matumizi wa fedha zao wanazopata katika kupunguza makali maisha.
Akizungumza na baadhi ya walengwa katika mitaa mbalimbali kwa nyakati tofauti Kabona amesema ni wajibu wa walengwa na watu wa karibu yao kuwashauri vema kufanya matumizi sahihi ya fedha wanazopewa ili kuleta nafuu katika kumudu mahitaji yao ya msingi.
" Nafahamu miongoni mwenu mmeanzisha vikundi vya kuchanga fedha na kukopeshana,ni jambo zuri.Leo mnapokea hela muhakikishe mnaweka akiba angalau kwa uchache kwa kuwa mpo wengi mnapigana tafu kwa baadae mnaeza kujadili pamoja vitu vya kufanya zaidi kutokana na makusanyo yenu.Tunahitaji mbadilike matumizi mabovu kama kulewa pombe hayana nafasi hapa ”.Amesema Kabona
Stella Makoye ni miongoni mwa walengwa yeye anaishi mtaa wa Nyasaka senta kata ya Nyasaka,ni mjane anasema ana watoto sita wote wapo shuleni anasema ana nafuu kubwa kwenye kuwahudumia watoto wake akisaidiwa na mradi wa ufugaji kuku aliouanzisha mwaka jana tangu alipoingia kwenye mpango.
“ Nashukuru serikali kupitia mradi huu watoto wangu kwa sasa wana uhakika wa kupata milo mitatu na kupata mahitaji yao yote madogo madogo ya msingi,Mungu awabariki sana muendelee kutuona mara kwa mara kama hivi.”
Zoezi la uhawilishaji fedha linaendelea ambapo jumla ya kiasi cha shilingi millioni 534.6 kwa ajili ya awamu mbili za malipo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 zinaendelea kutolewa kwa kaya 5868 za walengwa ndani ya Manispaa ya Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.