Katika kutekeleza shughuli za mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF inaunga mkono juhudi za serikali katika kutekeleza mkakati wa taifa unaolenga matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wake ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na ongezeko la uharibifu wa mazingira pamoja na athari za kiafya ,kiuchumi na kijamii zinazotokana na matumizi ya nishati isiyo safi kupikia.
Akizungumza wakati akitoa elimu kwa walengwa wa kata ya Kahama kutoka mitaa mitatu ya Magaka ,Kahama na Kadinda ambako kiasi cha shilingi 2,360,000 kimetolewa kwa kaya 103 mwakilishi wa TASAF ndugu Clavery Kazilo amesema “..ni jukumu la walengwa kubuni miradi ya nishati safi ya kupikia ngazi ya kaya kwa kuzingatia usalama wa nishati yenyewe sambamba na ubora wake,mkaa unaotokana na taka,umeme unaotokana na samadi ,msining’unike kuona ninyi ni wa tofauti sana na watu wengine bado mna nafasi ya kuwaza vizuri na kuja na kitu chenye manufaa kwenu na jamii nzima kwa ujumla..”
Nae mwenyekiti wa mtaa wa Magaka James Zabron amepongeza mpango wa TASAF kwa namna unavyofanya kazi kwa kusaidia wananchi wa mtaa wake kupeleka watoto shule na hospitalini kupata huduma za afya na kuendelea kukuza uelewa wao kwa namna mbalimbali zinazowawezesha kujikimu kimaisha huku akibainisha changamoto ya makato kupitia mifumo ya kieletroniki ambapo pesa za walengwa zinapitia.
“..serikali naomba ione namna bora ya kuondoa makato kwa walengwa kule wanakopitishia pesa zao kama ni kwenye simu au akaunti za benki ,baadhi ya walengwa hawataki kupokea fedha zao wakihisi wanaibiwa..” amesema mwenyekiti wa mtaa wa Magaka
Jumla ya kiasi cha shilingi milioni 128,712,968 zimetolewa kwa kaya 3,444 za walengwa wa TASAF ndani ya Manispaa ya Ilemela ambapo kaya 40 zinalipwa keshi kiasi cha shilingi 748,000 na kaya 3404 zinaendelea kulipwa kiasi cha shilingi 127,964,968 kwa njia ya simu na kupitia akaunti za walengwa wenye akaunti benki.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.